Arsenal yageuzwa kitoweo "EPL" yapigwa kipigo kingine.. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Sunday, 4 March 2018

Arsenal yageuzwa kitoweo "EPL" yapigwa kipigo kingine..

Klabu ya Arsenal imekubali kipigo kingine cha pili mfululizo kwenye michezo ya Ligi Kuu soka England, baada ya jioni ya leo kukubali kibano cha goli 2-1 dhidi ya Brighton & Hove Albion.

Magoli ya Brighton & Hove Albion yamefungwa na Lewis Dunk na Glenn Murray huku goli pekee la Arsenal likifungwa na Pierre-Emerick Aubameyang.

Mchezo uliopita Arsenali walikubali kipicgo cha goli 3-0 dhidi ya wababe wa EPL, Klabu ya Manchester City huku wakipoteza mchezo wa fainali ya kombe la EFL dhidi ya wababe hao.

Kwenye mchezo huo kama kawaida mashabiki wa Arsenal walikuwa wanaonesha mabango yaliyosomeka ‘WENGER OUT’ wakimshinikiza kocha wa klabu hiyo Mzee Wenger kuachia nafasi hiyo klabuni hapo.

No comments:

Post a Comment