Baada tu ya kushinda kesi yake dhidi ya lebo ya G-Worldwide na kuwa msanii huru, staa wa muziki Nigeria Kiss Daniel ameweza kusimamisha lebo yake binafsi ya Fly Boi Inc na kutangaza kununua nyumba yake ya pili.
Kiss Daniel ameonyesha jumba hili kwenye Instagram yake nakusema ana miaka minne tu kwenye muziki na haya ndio baadhi ya mafanikio yake.
Kiss ameandika “Asante Mungu nimwewza kununua nyumba ya pili mjini Lagos, Miaka minne tu kwenye hii biashara, Nawashukuru sana mashabiki zangu, Naomba wote tufanikiwe hivi AMEN #FBI #HAVENHOMES”
No comments:
Post a Comment