AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA KWA KUMBAKA BINTI WA MIAKA 9 - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Friday, 30 March 2018

AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA KWA KUMBAKA BINTI WA MIAKA 9

Mwanaume mmoja anaye tambulika kwa jina la Shadrack Majimbo mwenye umri wa miaka 42 mkazi wa Nakuru nchini Kenya amehukumiwa kifungo cha maisha ,jela kwa kosa la kumbaka binti mwenye umri wa miaka 9 na kumuambukiza magonjwa ya zinaa.

Hakimu Judicaster Nthuku amesema kuwa ushahidi unaonyesha kuwa mtuhumiwa huyo alifanya vitendo hivyo vya ubakaji, na ripoti ya daktari kuthibitisha hilo huku akimuambukiza ugonjwa wa zinaa aina ya ngono.
Mahakama imeelezea kwamba mtuhumiwa huyo alikuwa ni rafiki wa karibu wa familia ya binti huyo, ambapo siku ya tukio alimuita na kumtaka kumsaidia kazi za nyumbani, na ndipo alipomfanyia kitendo hicho cha ukatili na udhalilishaji.
Sambamba na hilo mwanaume mwengine mwenye umri wa miaka 74 aliyetambulika kwa jina la Kipngeno arap Bor katika eneo la Subukia nchini Kenya huko huko Nakuru, amehukumiwa miaka 10 jela kwa kosa la kumbaka mjukuu wake, ambaye mashahidi walimkuta akifanya tendo hilo baada ya kusikia kelele za binti huyo akilia na kuomba msaada.

No comments:

Post a Comment