Ray afunguka haya baada ya gumzo la kumvalisha mtoto wake heleni... - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Sunday, 18 February 2018

Ray afunguka haya baada ya gumzo la kumvalisha mtoto wake heleni...

Msanii wa filamu, Vincent Kigosi maarufu ‘Ray’ amesema kitendo cha kumvisha mtoto wake hereni ni kutokana na kuwa nyota kama yeye.

Ray amesema hayo alipozungumza na MCL Digital baada ya kuweka hadharani picha za mtoto huyo wa kiume aliyevishwa hereni hivyo kuzua gumzo. Maoni kadhaa yamekuwa yakitolewa kuhusu kitendo hicho pamoja na kunyolewa nywele staili ya kiduku.

Akizungumzia uamuzi wa kufanya hivyo kwa mtoto wake wa pekee aitwaye Jaden, msanii huyu aliyewahi kutamba na filamu za Oprah, Waves of Sorrow na Pretty amesema yeye ni nyota maarufu hivyo mtoto wake lazima afuate nyayo zake.

“Mbona mimi baba yake nimetoboa masikio watu hawasemi, si kwa kuwa wanajua mimi ni mtu maarufu, hivyo umaarufu huu nilionao hata mtoto lazima awe nao japo sijamtoboa sikio atakuja kufanya hivyo mwenyewe kama ataamua atakapokuwa mkubwa,” amesema.

Ray amesema, “Hao wanaosema waendelee tu kusema kwa kuwa kusema ni haki yao, na huyu ni mwanangu hakuna mtu wa kunipangia nini cha kumfanyia.”

No comments:

Post a Comment