Mimi Mars akili kufananishwa na Vanessa Mdee - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Friday, 2 February 2018

Mimi Mars akili kufananishwa na Vanessa Mdee

Msanii anayefanya vizuri kwa sasa ngoma ya 'Sitamani' chini ya Mdee Music, Mimi Mars amekubali yaishe kwa mashabiki wanaoendelea kumfananisha na dada yake Vanessa Mdee kwa kusema kuwa anaamini kufananishwa kwao hakutaisha hata akikataa kiasi gani.

Mimi Mars amekiri hayo wakati akipiga Story na Producer wa Planet Bongo ya East Africa radio, Grayson Gideon na kusema kwamba anafahamu ni ngumu sana kuwaaminisha watu kwamba yeye hafanani na Vanessa na yote ni sababu dada yake alikuwa wa kwanza kuingia kwenye muziki na watu wakamzoea sana.

Mimi Mars amesema kwamba awali alikuwa hapendi kusikia habari za kufananishwa na Vanessa lakini kwa sasa ameamua kuwaacha mashabiki wenyewe na siku wakiamua kumuona tofauti na Vanessa watafanya hivyo.

Mbali na hayo Mimi amejitetea kuwa tofauti yake na Vanessa Mdee  inatokana na yeye kuwa na sauti nzito, muonekano na hata uimbaji.

No comments:

Post a Comment