Feza kessy afunguka kumtongoza Mwanaume.. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday, 21 February 2018

Feza kessy afunguka kumtongoza Mwanaume..

Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye ametokea kwenye tasnia ya urembo, Feza Kessy, amekiri kuwahi kumtongoza mwanaume ambaye alitokea kumpenda, kitu ambacho ni kigumu kwa mabinti wengi.

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Feza amesema alipoachana na mpenzi wake aliyepita alikaa na upweke kwa muda mrefu, lakini alikuwa na hisia za mapenzi kwa msanii Cyril kwa muda mrefu tangu akiwa kwenye mahusiano ya awali, na kuamua kumwambia ukweli.

“Nilikuwa nam-like sana, yeye alikuwa anan-ilike kidogo, ye alitakiwa aje kunibembeleza kiukweli maana kipindi kile nilikuwa naupweke plus kuumizwa, nilikuwa natangaza nia kwakweli lakini akawa ananiambia ooh sijui nina mtu, sasa na mimi nikawa siamini nilidhani ananipima kwanza, lakini ndio ikawa hivyo hata mtu wake akanifuata inbox kunitaka niachane naye”, amesema Feza Kessy.

Pamoja na kutoswa huko kutoka kwa Singida Boy mwenye Six Pack Zake, Feza amesema wamebaki kuwa marafiki wazuri, lakini bado ana hisia za kweli kwa Cyril na sio kumzingua.

No comments:

Post a Comment