Kocha Joseph Omog amekerwa na ushindi wa mbinde. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Monday, 2 October 2017

Kocha Joseph Omog amekerwa na ushindi wa mbinde.

Kocha Mkuu wa Simba, Mcameroon, Joseph Omog, ametoa maagizo kwa wachezaji wa kikosi hicho kuhakikisha wanapata ushindi kwenye michezo yao ya sasa ili kutumia vizuri nafasi ya matokeo ya wapinzani wao ambayo yamekuwa ya kusuasua.

Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog amekwenda kushusha ukali wa mazoezi.
Azam juzi ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Singida United kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, wakati Yanga na Mtibwa Sugar zilitoka suluhu kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Omog, kabla ya jana Jumapili hawajacheza na Stand United mkoani Shinyanga, alikuwa ameiongoza Simba kushinda kwenye michezo yake miwili kati ya minne waliyoshuka dimbani huku wakitoka sare kwenye michezo miwili.
Mkuu bosi huyo wa benchi la ufundi la Simba, amesema kuwa ni lazima wachezaji wake watumie vyema kipindi hiki ambacho wapinzani wao wakubwa hawapati mataokeo mazuri kushinda mechi zao kwa ajili ya kuepuka presha wakati ligi ikiwa inaenda mwishoni.

“Kwa sasa tunatakiwa kutokuwa na masihara kabisa ndani ya dakika 90 za kila mchezo wetu, tupambane kupata ushindi kwa njia yoyote ile na wachezaji wanatakiwa kujitoa kulifanikisha hilo, nasema hivyo kwa sababu ukiangalia wapinzani wetu wengi hawapati yale matokeo mazuri sasa hiyo inatakiwa iwe faida kwetu.

Omog aliendelea kusisitiza
“Kama tukiwa tunafanya vizuri na kushinda mechi zetu kwa sasa tutatengeneza gepu la pointi na wenzetu ambao hawana matokeo mazuri, lakini pia itatusaidia kuepuka ile hali ya presha wakati ligi ikiwa inaenda mwishoni kuanza kuangalia mpinzani wako nini ambacho anakifanya kama ilivyokuwa imetokea msimu uliopita,” amesema Mcameroon huyo.

No comments:

Post a Comment