Bado siku 30 Diamond na Zari kuandika historia kubwa kuliko.. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Sunday, 18 February 2018

Bado siku 30 Diamond na Zari kuandika historia kubwa kuliko..

Wachumba wa Zamani Diamond Platinumz na Zari wanatarajia kuandika historia nyingine kama ilivyo kawaida yao pale uwanja wa uhuru ambapo kutakuwa na matukio mengi sana ikiwemo album ya mwanamuzi Diamond Platinumz " A boy from Tandale" ambayo kwa tukio la kuzindua inataraji kuuza nakala 30,000 za mwanzo huku kukiwa na kiingilio kuwaona wasafi wote wakiongozwa na Diamond Platinumz.

Hata hivyo waandaaji wa tukio hili walishaomba uwanja wa taifa lakini wameambiwa utakuwa na matumizi hivyo wamepewa uwanja wa uhuru kwani kwa makisio yao waliona uwanja wa uhuru hautotosha kabisa lakini Plan imekuwa ni kufanya tukio hilo kila mkoa kwa kiingilio ambacho hakitasababisha watu kushindwa kupumua uwanjani.....

Katika siku hiyo kutakuwa na tukio lingine kubwa zaidi ambalo sitaliweka hapa kwa sababu za kibiashara lakini joto la tukio hilo litapanda zaidi ikifika march kwani kuna mengi zaidi yatatangazwa kuhusu Diamond na kuwaacha wengi midomo wazi....

Kikubwa zaidi ni kuwa tamasha hili hadi sasa linagombewa na kampuni kubwa mbili ambazo zinataka kuweka matangazo mule ndani ya uwanja siku ya tamasha ambalo bila shaka litaweka historia......

Wana jamvi kwa leo nawajuza haya tuu lakini mkumbuke kuwaona Diamond na Zari safari hii ni kwa pesa si bure tena

No comments:

Post a Comment