WAKONGWE wa Ligi Kuu Bara klabu za Simba na Yanga leo hii kuanzia jioni, kwa nyakati tofauti watacheza mechi za Kombe la Mapinduzi kwenye Uwanja wa Amaan, Kisiwani Zanzibar.
Yanga itakuwa inacheza mechi yake ya pili tangu ilipotua Zanzibar dhidi ya JKU ya Unguja saa 10:30 jioni, hii ni baada ya kupata ushindi kwenye mchezo wao wa kwanza wa 2-1 dhidi ya Mlandege ya Unguja.
Kwa upande wa Simba ambayo ilianza mashindano hayo vibaya baada ya kutoa sare ya 1-1 na Mwenye ya Pemba, itaingia uwanjani kukipiga na Jamhuri ambayo pia inatoka Pemba saa 02:15 usiku.
Wachezaji na benchi la ufundi la kikosi hicho, wametamba kuifunga Jamhuri, kwani baada ya kufanya makosa kwenye mchezo wao na Mwenye, hawataki kurudia.
No comments:
Post a Comment