Msanii Suzan Michael maarufu kama Pretty Kind amefunguka na kuomba radhi kwa Serikali na Watanzania kwa ujumla kutokana na vitendo vyake vya kupiga na kuweka picha mitandaoni za nusu uchi.
Akiongea leo Januari 7, 2018 baada ya kufungiwa na serikali kujihusisha kufanya kazi zozote za sanaa kwa miezi sita, Pretty Kind amesema kuwa amejifunza na kugundua kuwa alikuwa anafanya makosa hivyo sasa hataweza kurudi tena kufanya mambo hayo.
"Naomba niombe radhi kwa Watanzania wote kwa hiki nilichokifanya natambua nimefanya kosa naomba msamaha aweze kunisamehe, pia naomba msamaha kwa mashabiki zangu kwa hiki kilichotokea nimejifunza hivyo nitakuwa Pretty Kind mwingine mpya na kufanya yale yanayotakiwa katika jamii" alisema
Pretty Kind amefungiwa kujihusisha na sanaa kwa takribani miezi sita baada ya kuposti picha katika mtandao wake wa Instagram ikimuonyesha akiwa nusu utupu jambo ambalo ni kinyume na maadili ya Kitanzania na kwenda kinyume na maagizo ya Rais John Pombe Magufuli ambayo aliyatoa hivi karibuni kuwataka wasanii wa kike kuvaa kwa staha.
No comments:
Post a Comment