Kikosi cha Simba kilichopo chini ya Kocha Masoud Djuma, kinaendelea na mazoezi jioni ya leo Jumapili kwenye Uwanja wa Nyuki, Zanzibar.
Simba jana walipoteza mechi dhidi ya Azam FC katika hatua ya makundi na ili kusonga mbele wanatakiwa kuwafunga URA.
Wachezaji wa Simba walionekana wakifanya mazoezi makali katika Uwanja wa Nyuki ili kuhakikisha wanajiweka fiti kwa ajili ya mchezo wa kesho Jumatatu.
Hata hivyo, Simba wana nafasi ya kusonga mbele huku wakitakiwa kuibuka na ushindi mbele ya Waganda hao ambao mchezo wao wa hivi karibuni waliifunga Azam FC.
Job Opportunity At Uganda Airlines- Security Manager
-
*About US:*
Uganda Airlines is the National Carrier of the Republic of Uganda based at
Entebbe International Airport. It is headquartered in Entebbe, Waki...
No comments:
Post a Comment