Naibu Waziri amtaka mkandarasi kufika ofisini - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Sunday 7 January 2018

Naibu Waziri amtaka mkandarasi kufika ofisini

Mbeya. Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgandu amemtaka mkandarasi wa Kampuni ya State Grid Electrical and Technical Works ambaye ni wakala wa kusambaza Mradi wa Nishati Vijijini (Rea), mikoa wa Mbeya na Songwe kufika ofisini kwake Dodoma kutoa maelezo ya kushindwa kukamilisha mradi huo kwa wakati.

Mgandu alitoa amri hiyo jana mkoani hapa baada ya kufanya ziara ya kikazi wilaya za Mbeya na Kyela na kubaini mkandarasi huyo amekuwa akifanya kazi bila kujali muda.

“Haiwezekani tukaenda kwa mwendo huu, wananchi wanasumbuka sana kutafuta huduma ya umeme, ninakutaka ufike ofisini kwangu ndani ya siku saba kuanzia leo (jana) utoe maelezo kwa nini mpaka sasa hujakamilisha kusambaza umeme katika vijiji vilipangwa katika awamu ya pili kwa zaidi ya mwaka moja,” alisema Mgandu.

Alifafanua kuwa Serikali itahakikisha inawachukulia hatua za kisheria makandarasi wanaorudisha nyuma azma ya Rais John Magufuli ya kuwafikishia umeme wananchi ifikapo mwaka 2021.

Kaimu Meneja wa miradi ya Rea Mbeya, Emmanuel Yesaya alisema vijiji zaidi ya 150 vimelengwa kufikiwa na umeme katika awamu ya tatu kwa 2018/19 na kwamba taasisi za Serikali kama shule, zahanati na visima vya vijiji vitapewa kipaumbele.

Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mkoa wa Mbeya, Benedict Bahati alisema mkandarasi huyo sehemu kubwa ya utekelezaji wake umekuwa ni wa chini ya kiwango.

No comments:

Post a Comment