BENCHI la ufundi laYanga, limemkabidhi kazi maalumu straika wake, IbrahimAjib kupiga mipira yote ya adhabu, kona pamoja na penalti.
Ajibu tayari amefunga mabao mawili kwa mipira ya adhabu, jambo ambalo limelivutia benchi la ufundi la klabu hiyo kuamua kumpa kazi hiyo.
Katika mchezo wa juzi Jumatano dhidi ya Mwadui FC, Ajib ndiye alikuwa mpigaji mkuu wa kona na faulo na moja kati ya pigo lake lilipanguliwa nakipa wa Mwadui nakugonga mtambaa wa panya.
Kocha msaidizi wa timu hiyo, Shadrack Nsajigwa alisema Ajib amepewa kazi hiyo ndio maana alikuwa anawajibika kila ilipokuwa ikitokea faulo ama kona kwenye mechi hiyo ya Mwadui
“Kona na faulo alizokuwa anapiga Ajib sio kwamba alijiamulia, bali yalikuwa ni maelekezo ya benchi la ufundi, ndio maana alikuwa shapu kutimiza wajibu wake,” alisema.
Katika hatua nyingine, Nsajigwa alisema wali lazimika kumtumia staa wao, Amissi Tambwe kwa dakika49 tu dhidi ya Mwaduikwa kuwa alikuwa ametokakuugua homa kali nabado hajawafiti kwa asilimia zote.
“Mchezaji ametokakuumwa huwezi kuanzanaye kwa kasi, muda aliotumika ulikuwasahihi kwake na ndiouliopangwa acheze.Tambwe akiwafiti zaidi ataisaidiaYanga,” alisema.
Tambweraiawa Burundi alikuwa tegemeo katika safu ya ushambuliaji ya Yanga kwa kupachika mabao, awali alikuwa na matatizo ya goti ambayo yalimuwekanje kwa muda mrefu. Mara ya kwanza kumtumia ilikuwa ni katika mechiya Kombe laFA dhidi ya REHA.
Job Opportunity At Uganda Airlines- Security Manager
-
*About US:*
Uganda Airlines is the National Carrier of the Republic of Uganda based at
Entebbe International Airport. It is headquartered in Entebbe, Waki...
No comments:
Post a Comment