Pretty Kindy hakuna wa kunilinganisha na Amber Lulu - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Thursday 9 November 2017

Pretty Kindy hakuna wa kunilinganisha na Amber Lulu

Video queen na muigizaji wa Bongo Movies anayekuja kwa kasi Bongo, Pretty.

MSANII wa Bongo Fleva ambaye pia ni video queen na muigizaji wa Bongo Movies anayekuja kwa kasi Bongo, Pretty Kindy ameweka wazi kuwa, kwa upande wa mavideo queen ambao wametimkia kwenye muziki akiwemo Amber Lulu, hakuna wa kumlinganisha nao.

Amber Lulu

Akichonga  Pretty Kindy alisema kuwa, hawezi kukimbia kuwa video queen kama walivyofanya akina Amber Lulu, Gigy Money na wengine kwa sababu anajiamini na analipwa vizuri na kwamba hata kwenye muziki hajaona wa kumpa changamoto.

“Kiukweli hakuna wa kunilinganisha na hao wengine, juzikati nilikula dili la uvideo queen kwenye ngoma ya Benny Kinyaiya na nililipwa vizuri sana, lakini siwezi kuikimbia tasnia hiyo, kisa malipo, maana kama ni fedha ninajua nitalipwa za kutosha,” alisema mwanadada huyo ambaye amewahi kushiriki kwenye muvi za Damu Yangu ya Riyama Ally na Who Is Back ya Baba Haji.

No comments:

Post a Comment