Lwandamina:Bado nipo nipo kwanza! - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday, 15 November 2017

Lwandamina:Bado nipo nipo kwanza!

KOCHA mkuu wa Yanga, Mzambia George Lwandamina ameweka wazi kuwa suala la kujiunga na klabu ya Zesco ni uvumi tu kwa sababu watu wanapenda kuzungumza. 

Lwandamina ametua nchini jana akitokea kwao Zambia alikoenda kuhani msiba wa ndugu yake. Amesema: "Watu wanazungumza kwa sababu wanapenda kuzungumza, nimesikia lakini huo ni uvumi tu nilikwenda Zambia kwa mambo mengine kabisa." Lwandamina alitoa kauli hiyo kutokana na madai kuwa, safari yake ya Zambia ilikuwa ni pamoja na kufanya mazungumzo na klabu ya Zesco aliyokuwa anaifundisha miaka ya nyuma kabla ya kujiunga na Yanga. Hata hivyo, kikosi cha Yanga kilifanya mazoezi asubuhi ya leo hii Uwanja wa Uhuru bila Lwandamina.

No comments:

Post a Comment