Ajibu,Yondani waifanyizia Simba - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Friday, 17 November 2017

Ajibu,Yondani waifanyizia Simba

KAMARI iliyoicheza Simba kuwaachia mastaa muhimu kwenda Yanga imeiponza. Ilianza na Kelvin Yondani, Amissi Tambwe na sasa Ibrahimu Ajibu, wote wameibeba Yanga huku rekodi zikionyesha mastaa wa zamani wa Msimbazi ndiyo kikwazo kwa Wekundu hao kubeba taji hilo lenye heshima zaidi nchini.

Simba ilikuwa imelishika zaidi soka la Tanzania mwanzoni mwa miaka ya 2000, lakini tangu imeanza kuachia mastaa wake kujiunga na Yanga, mambo yamekuwa tofauti kabisa.

Ilianza kama utani mwaka 2008 ambapo aliyekuwa kipa wao mahiri Juma Kaseja akaenda Yanga na kuisaidia kuondoka na taji la Ligi Kuu msimu wa 2008/9.

Simba ikafanya kosa jingine mwaka 2012 kwa kumuachia aliyekuwa beki wao kisiki, Yondani kutua Yanga na tangu hapo taji la Ligi Kuu wamekuwa wakiliona kwenye televisheni tu.

Yondani mara baada ya kutua Yanga, aliisaidia timu hiyo kushinda taji la Ligi Kuu mwaka 2013 kabla ya kulipoteza kwa Azam mwaka uliofuata. Tangu ameondoka Simba, Yondani tayari ameshinda mataji manne akiwa Yanga.

Kabla ya kutua Yanga, Yondani alikuwa ameshinda mataji matatu ya Ligi Kuu na Simba, hivyo ni kama ameiachia gundu timu hiyo inayofikisha miaka sita bila kutwaa taji hilo.

Mwaka 2014, Simba ilifanya kosa jingine tena kwa kuachana na staa mwingine Tambwe ambaye alikuwa Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2013/14. Tambwe alitua Yanga na mwaka 2015 aliisaidia kubeba taji la Ligi Kuu akifunga mabao 13. 

Mrundi huyo alipigilia msumari wa moto kwa Simba baada ya kuibeba tena Yanga msimu uliofuata kwa kuipa taji jingine huku akiibuka Mfungaji Bora kwa mabao 21.

Msimu huu, Simba imempoteza straika matata, Ajibu, ambaye ndiye kinara wa mabao kwa Yanga sasa akiwa amefunga mara tano na kuisaidia timu hiyo kuendelea kuwa na matumaini ya kutwaa ubingwa.

Kama historia itajirudia kwa ilivyokuwa kwa akina Yondani na Tambwe, huenda Ajibu akawa chanzo kikubwa cha Simba kupishana na taji hilo msimu huu tena.
Ajibu kwa sasa ametengeneza pacha imara ya mabao sambamba na Obrey Chirwa, kwa pamoja wameifungia timu hiyo mabao manane.

MAKOCHA WANENA
Aliyekuwa Meneja wa timu ya vijana ya Simba iliyowaibua akina Jonas Mkude, Said Ndemla na Ajibu, Patrick Rweyemamu alisema: “Siku zote nia ya kushiriki mashindano ni kutwaa ubingwa, kwa sasa Simba imetimia zaidi, wachezaji wazuri wote wapo Simba na kufanya vizuri ama vibaya inategemea na wao wenyewe.”

Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, alisema: “Mara nyingi Yanga huwa inatazama wachezaji wazuri kutoka Simba, ndiyo maana wanaokuja wanafanya vizuri.

“Lakini wakati mwingine usajili ni kamari, kuna waliokuja Yanga miaka ya nyuma wakitokea Simba na hawakufanya vizuri

No comments:

Post a Comment