Yanga yaonyesha mbwembwe zao leo Tabora Simba wamedata! - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday, 18 October 2017

Yanga yaonyesha mbwembwe zao leo Tabora Simba wamedata!

Dar es Salaam. Timu ya Yanga imetoka sare na Rhino Rangers kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora leo Jumatano.

Timu hizo zilionyesha ufundi, huku Yanga ikiwatumia zaidi wachezaji wa kikosi cha pili na wachache kutoka kikosi cha kwanza.

Mechi hiyo ya Yanga ni maandalizi kuelekea mchezo wa wikiendi dhidi ya Stand United na mechi ya Oktoba 28 itakayowakutanisha na watani zao Simba.

Beki wa Yanga Hassan Kessy alisema kwamba mchezo huo anaamini kocha wao atautumia kufanya maboresho ya kikosi cha kwanza kulingana na kile alichokiuona kabla ya mechi zinazofuata.

No comments:

Post a Comment