Chirwa,Ajibu waifanya kitu mbaya Kagera Sugar - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Saturday, 14 October 2017

Chirwa,Ajibu waifanya kitu mbaya Kagera Sugar

Dar es Salaam. Yanga imepaa kileleni mwa msimamo wa ligi kwa mara ya kwanza baada ya kuichapa Kagera Sugar mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba.

Mabingwa hao watetezi wamefikisha pointi 12 na kuwashusha vinara Simba wenye pointi 11 hadi nafasi ya tatu kabla ya mchezo wao wa kesho Jumapili dhidi ya Mtibwa Sugar.

Azam nayo imesogea nafasi ya pili ikiwa na pointi 12 baada ya kukubali kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Mwadui jana ugenini.

Kwenye Uwanaj wa Kaitaba, mabao ya Obrey Chirwa na Ibrahim Ajib yalitosha kuifanya Yanga ikae kileleni kwa ligi kwa mara ya kwanza tangu msimu huu uanze huku ikiacha machungu kwa wenyeji Kagera Sugar ambao hawajashinda mechi yoyote msimu huu.

Katika mchezo wa leo Yanga ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 40 lililofungwa kwa shuti kali na Obrey Chirwa aliyemalizia pasi ya Ibrahim Ajib na kuwafanya mabingwa hao watetezi kwenda mapumziko wakiongoza kwa bao 1-0.

Dakika mbili baada ya kuanza kipindi cha pili, Ajib akaipatia Yanga bao la pili kwa shuti kali akimalizia pasi ya Chirwa na mchezaji huyo kuvua jezi na kwenda kuionyesha kwa mashabiki na kuambulia kadi ya njano kutoka kwa mwamuzi Andrew Shamba wa Pwani.

Kuingia kwa bao hilo kuliwaamsha Kagera Sugar na kufanikiwa kupata bao dakika ya 52 lililofungwa na Jafari Kibaya kwa kichwa akitumia makosa ya kipa wa Yanga, Youth Rostand aliyechelewa kucheza krosi ya Mwaita Gereza.

Matokeo hayo yameifanya Kagera Sugar kuendelea kushika mkia baada ya kutopata ushindi katika michezo sita iliyocheza hadi sasa jambo lililoonekana kumuhuzunisha kipa namba moja wa timu hiyo Juma Kaseja ambaye alionekana kusikitika baada ya kmchezo huo.

Matokeo mengine, Azam ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Mwadui katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Mwadui Complex Shinyanga. Azam ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 9 kwa penalti lililofungwa na Himid Mao kabla ya Hassan Kabunda kuisawazishia Mwadui.

Kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara wenyeji Ndanda walitoka sare ya bao 1-1 na Majimaji. Willium Lucian'Gallas' alikuwa wa kwanza kuipatia Ndanda bao kwa mkwaju wa penalti dakika ya 35 kabla ya Majimaji kusawazisha dakika ya 45 kupitia kwa Aziz Sibo.

Kwenye Uwanja wa Mabatini Pwani, Ruvu Shooting ilitoka suluhu na Singida United wakati Uwanja wa Sabasaba Njombe,wenyeji Njombe Mji walitoka suluhu na Lipuli.

Msimamo Ligi Kuu Tanzania Bara 2017-2018

P W D L F A PTS

1. Yanga  6 3 3 0 6 3 12

2. Azam 6 3 3 0 5 2 12

3. Simba 5 3 2 0 14 3 11

4.Mtibwa   5 3 2 0 5 2 11

5.Singida 6 3 2 1 6 4 11

6.Prisons 5         2 3 0 8 5 9

7.Mbeya 6      2 2              2 7 7 8

8.Ndanda 6 2 2 2 4 4 8

9.Mbao 6 1 3 2 8 9 6

10.Lipuli 6 1              3 2 3 4 6

11.Njombe 6 1 2 3 3 5 5

12.Mwadui6 1 2 3 6 11 5

13.Ruvu 6 0 5 1 3 10 5

14.Majimaji6 0 4 2 4 6 4

15. Stand 5         1 0 4 3 6 3

16.Kagera  6 0 2 4 2 6 2

No comments:

Post a Comment