Simba inamnyemelea mchezaji huyu wa uingereza - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Friday, 20 October 2017

Simba inamnyemelea mchezaji huyu wa uingereza

Mlinda mlango Abbas Pira aliyekuwa anadakia timu ya Wrexham FC ya Uingereza inayoshiriki Ligi Daraja la Tatu (Conference Legue), ameamua kuachana nayo kutokana na majeraha yanayomkabili.

Kwa sasa mchezaji huyo yupo nchini kwa mapumziko na ameeleza kuwa tayari kuna timu tatu za hapa nchini zimeonesha nia ya kuhitaji huduma yake ikiwemo Simba, Mtibwa na Mbeya City na nyingine mbili kutoka nje ya nchi.

Pira aliyeanzia soka katika timu ya Coastal Union, alisema aliingia mkataba wa mwaka mmoja na timu hiyo lakini alidumu kwa mwezi mmoja na nusu pekee kabla ya kuwa nje ya uwanja kutokana na majeraha yanayomkabili.

“Miaka ya nyuma nilivunjika mguu hivyo katika matibabu kuna kipande cha chuma kipo mguuni na wakati nikiendelea na majukumu yangu, nilijitonesha hivyo daktari alishauri nifanyiwe tena upasuaji au kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu na nimekubali kukaa nje kuliko kufanyiwa upasuaji,” alisema Pira.

Alisema, “Siwezi kusema nakwenda timu gani nikipata nafuu, kwani timu zote zimeonesha nia nzuri kwangu na mimi pia nahitaji kuangalia kwa mapana zaidi katika kupiga hatua kwenye soka.”

No comments:

Post a Comment