Niyonzima afunguka haya hapa kuhusu Simba - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Thursday, 19 October 2017

Niyonzima afunguka haya hapa kuhusu Simba

Kiungo Haruna Niyonzima amesema kamwe hawezi kuidharau Simba kama ambavyo baadhi ya watu wanataka kuonyesha.

Niyonzima amesema yeye ni mtu anayejitambua na anaelewa afanye nini, hivyo ataendelea kuiamini na kuithamini Simba kwa kuwa ndiye mwajiri wake.
“Siwezi kuidharau Simba hata kidogo kwa kuwa ndiyo inajua ninaishi vipi, ndiyo inanipa mshahara.

“Simba ndiyo ofisi yangu, hivyo ni lazima niiheshimu. Jamani mpira sio vita. Baada ya mpira sisi ni binadamu hivyo hatupaswi kuonyesha kama ni adui au ambao hatuwezi kuwa pamoja,” anasema.

No comments:

Post a Comment