Dar es Salaam. Mshambuliaji Donald Ngoma ataukosa mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar kutokana na kuwa majeruhi ya misuli ya paja.
Balaa la majeruhi limezidi kuiandama Yanga kwani tangu msimu huu kuaanza mastaa wengi wamekuwa wakipokezana kupata majeraha hivyo kuathiri kiwango cha mabingwa hao watetezi.
Alianza mshambuliaji, Amiss Tambwe pamoja na kipa Beno Kalolanya, Obrey Chirwa kisha akafuatia Kamusoko na sasa ni Ngoma.
Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano cha Yanga, Dismas Tena amethibitisha kuwa Ngoma hatasafiri na wenzake kesho kwenda Bukoba kwa ajili ya mchezo huo.
Ngoma ni mmoja wa wachezaji walioiongoza Yanga kuishushia mvua ya mabao Kagera Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu msimu uliopita kwenye mzunguko wa pili, baada ya kuifunga mabao 6-2 huku yeye akitupia wavuni mabao mawili, mengine yalifungwa na Obrey Chirwa (2), Simon Msuva na Deus Kaseke.
No comments:
Post a Comment