Lady Jay Dee na Mwana FA wamaliza tofauti zao baada ya kuwa na bifu kubwa - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Thursday 12 October 2017

Lady Jay Dee na Mwana FA wamaliza tofauti zao baada ya kuwa na bifu kubwa


Msanii Lady Jaydee ambaye hivi karibuni amepatana na aliyekuwa mhasimu wake msanii Mwana FA, amesema alishukuru sana kwa kitendo cha Mwana FA kumpa ushirikiano kwenye kazi zake na kupost Instagram kumpa promo.

Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Lady Jaydee amesema ni jambo jema na la kumshukuru Mungu kwa wasanii wanapopeana ushirikiano.

“Ni jambo jema msanii mwenzako anapokusuport, na ndio kitu ambacho wasanii wengi tunapenda, sisi binadamu kwa hivyo mkae mkifahamu kwamba hakuna marefu yasiyo na ncha, nilishukuru kwamba msanii mwenzangu amenisuport”, amesema LadyJaydee.
LadyJaydee ameendelea kwa kusema

kwamba.... “ni wasanii ambao tulikuwa tunaelewana, na ndio maana tuliweza kufanya nyimbo nyingi ambazo ziliweza kufanya vizuri, watu walikuwa wanasikitika kwa yale yaliyotokea”.

Wawili hao walikuwa kwenye bifu kali ambalo ilikuwa hata salamu hakuna, lakini hivi karibuni wameamua kuyamaliza na kuondoa tofauti zao.

No comments:

Post a Comment