Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amesema kamwe hawezi kutoa siri ya kwanini hawezi na hatokuja kuifundisha klabu ya Barcelona.
Mourinho ameyasema hayo muda mfupi baada ya kuthibitisha kuwa hatamalizia taaluma yake ya kufundisha soka ndani ya klabu ya Manchester United ambapo amesema kuna sehemu nyingi na mambo mengi hajayakamilisha hivyo ipo siku atahitaji changamoto mpya.
Katika mahojiano na runinga ya Telefoot Mourinho aliulizwa ni timu gani siku moja angependa kuifundisha ambapo alijibu “Zipo timu nyingi ila mtoto wangu mmoja anapenda kuisifia PSG na wikiendi iliyopita alisafiri kutoka London kwenda Ufaransa kutazama mechi ya PSG akaacha mechi ya Manchester na Liverpool hivyo inaonesha PSG ina vitu vizuri”.
Mtangazaji akamuuliza kwanini hafikirii kuifundisha Barcelona Mourinho alisema “ Vipo vitu ni siri ya maisha yangu ya ukocha na vitabaki kuwa siri yangu, labda ipo siku nitasema nikiwa mzee tena mzee sana”.
Mourinho amewahi kuwa kocha msaidizi wa Barcelona chini ya Bobby Robson na Louis Van Gaal kati ya mwaka 1996 na 2000 ambapo walifanikiwa kutwaa ubingwa wa La Liga mara mbili.
Job Opportunity At Uganda Airlines- Security Manager
-
*About US:*
Uganda Airlines is the National Carrier of the Republic of Uganda based at
Entebbe International Airport. It is headquartered in Entebbe, Waki...
No comments:
Post a Comment