hii ndiyo safari ya muziki ya Rosa Ree - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Saturday 21 October 2017

hii ndiyo safari ya muziki ya Rosa Ree

Staili ya kubinua midomo iliyokolea rangi nyeusi, mitindo ya nywele ya aina yake na vivazi vinavyoacha sehemu kubwa ya mwili wake vinamtambulisha vyema Rosa Ree.

Rapa huyo anayewakilisha kina dada katika gemu alitambulishwa na ngoma yake ya kwanza One Time akiwa tayari ameshaingia mkataba na lebo ya The Industry.

Mwanadada huyo ambaye jina lake halisi ni Rosary Robert Iwole kama wanamuziki wengine naye safari yake imeanzia mbali. Mwenyewe anasema haikuwa rahisi kama tembo kulitafuna bua…ilijaa mabonde na milima.

Mpaka sasa ameachia ngoma tatu ambazo zinakimbiza ambazo ni One Time, One Time remix ambayo alifanya na rapa kutoka Kenya, Khaligraph Jones, Up In The Air na kazi ya Mchaga Mchaga ambayo amewashirikisha mabosi zake kundi la Navy Kenzo.

Dili na The Industry?

“Muziki nilianza muda mrefu, yaani tangu nikiwa shule na tena nilikuwa naimba. Kuna ngoma kadhaa nilitoa ambazo nilikuwa naimba lakini hazikufanya poa,”
“Nilianza kuchana nikakuta watu wanapenda sana nikaamua kukaa humo. Mwaka 2015 nilienda kwa Nahreel kurekodi ngoma alivyonisikia tu alipenda sana. Baadae aliniomba niwe kwenye lebo yake nilifurahi sana kwanza halafu sikuamini lakini ikawa hivyo nikasaini hapo, mpaka sasa napiga mzigo,”
Mishe nyingine?

“Mimi nafanya biashara pia lakini mambo yangu mimi napenda kuyaweka kwa siri hivyo siwezi kusema ni biashara gani mpaka mambo yangu fulani yatimie,” aliongeza.

Nini kinafuata baada ya Mchaga Mchaga?
“Baada ya Mchaga Mchaga kuna ngoma kali inakuja yani hapa nasubiri tu wakati uwadie kitu tukiachie, pia, nafikiria kutowachosha mashabiki zangu sababu nataka kuachia ngoma kali kwa kila kipindi fulani,” alisema.

“Na pia kuhusu video ya Mchaga Mchaga mipango bado ipo inafanyika ili kuja na kitu tofauti kama unavyojua Rosa Ree tangu nitoke kwenye upande wa video nikiri sijawahi kuzingua na hivyo najipanga kuja na jiwe kali sana.” Kolabo na Rapa wa Kenya?

“Aisee hii kolabo nikiri imenipa mafanikio makubwa sana,kwanza imeniongezea sana mashabiki kwa upande wa Afrika Mashariki kwa ujumla na mafanikio mengine ambayo siwezi kuyaweka wazi ila kiukweli nimepata mafanikio niliyotarajia,” Amesema.

Staili yake vipi?

Moja ya jambo kubwa ambalo mara kadhaa amekuwa akikumbana nalo ni watu kadhaa wamekuwa wakimkosoa hasa staili yake ya mavazi wakidai yapo nje ya maadili ya Kitanzania pamoja na matumizi ya maneno katika nyimbo zake ambayo yamejaa matusi sana.

“Mimi sifikirii hata kidogo kubadilika sababu eti kwa maneno ya watu sababu kuwa orijino ndicho kitu cha msingi halafu ukifuata kila kitu watu wanasema ni kazi sana kufanikiwa cha msingi mi sitobadirika bali nitazidi kuwa bora zaidi sababu naamini kuna watu wanapenda ninachokifanya,”

Watu wasichojua kutoka kwake?

“Kuna vingi wengi hawajui kutoka kwangu, huwa wanaweka vitu vyao kutokana na namna wanavyoniona, lakini kiukweli mimi napenda sana sana watoto na situmii kilevi chochote kuna watu huwa hawaamini lakini ukweli ndio huo,”
Kama si Muziki basi angekuwa anafanya nini?

“Ningekuwa daktari aisee kama sio muziki maana ni kitu ambacho kilikuwa akilini mwangu kwa hiyo kama nisingekuwa nafanya muziki basi ningekuwa nachakarika na wagonjwa Hospitalini,”
Shoo ambayo hatokuja kusahau.

“Sitokuja kusahau shoo ya “Castle Lite Unlock” ki ukweli shoo nyingi huwa napata shangwe sana ila hiyo shoo nakumbuka nilipafomu wimbo wa Mchaga Mchaga ambao ulikuwa bado haujatoka na watu walikuwa wakiitikia ilinipa sana nguvu asikwambie mtu,”
Vitu ambavyo hapendi kuja kuvifanya kabisa
“Kitu ambacho sifikiri kabisa kuja kufanya ni siasa,mimi sipendi kabisa siasa na sifikiri kabisa sijui kwa mbele itakuaje ila akili yangu inaniambia hivyo kwamba Rosa Ree siasa wewe kwako haipo,”

Albamu na Mixtapes (Kanda Mseto) vipi?
“Mipango ipo sema nafikiri bado mashabiki zangu wanahitaji singo zaidi ili kuwatengenezea nafasi ya kuja kufurahia albamu yangu ila mipango ipo na pindi itapowadia watu wataona.”

No comments:

Post a Comment