Breaking:Mayanja amejiuzulu kuifundisha Simba - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday, 18 October 2017

Breaking:Mayanja amejiuzulu kuifundisha Simba

Dar es Salaam. Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja amejiuzulu kuifundisha timu hiyo, huku akiweka bayana kwamba ni kutokana na sababu za kifamilia.

Tangu jana Jumanne usiku kulikuwa na taarifa za kufukuzwa kocha huyo na uongozi wa klabu hiyo, lakini tayari ameweka wazi jambo lililomsukuma kuachana na Wekundu hao wa Msimbazi.

Mayanja ameachia ngazi, huku Simba ikiwa inaongoza kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 12 sawa na wapinzani wao Yanga, lakini wakizidiana mabao ya kufunga na kufungwa.

Kikosi cha Simba kinatarajia kuikaribisha Njombe Mji kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam wikiendi hii.

No comments:

Post a Comment