NANDY AMEFUNGUKA BIFU LAKE NA RUBY. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Sunday 10 September 2017

NANDY AMEFUNGUKA BIFU LAKE NA RUBY.

Nandy.
MSANII wa Bongo, Faustina Charles ‘Nandy’ amesema kuwa, japo watu wengi wamekuwa wakijadili kuhusu ukaribu wake na msanii wa zamani zao la Jumba la Kuibua Vipaji (THT), Ruby kwa madai kuwa kwa sasa hawapikiki chungu kimoja kutokana na ushindani uliopo baina yao, ishu hiyo si kweli kwani hana bifu na mwanadada huyo.
Ruby.
Nandy alizungumza kuwa, anawashangaa wanavyosema hapatani na Ruby kwa madai kuwa anachukiwa kwa sababu amemfunika mwenzake kimuziki.
“Ukiniuliza mimi na Ruby nani anaimba vizuri, nitakujibu wote, yeye ana muziki wake nami nina wangu, sina ugomvi wala mazoea naye ila tukukutana tunasalimiana tu kama washikaji,” alisema

No comments:

Post a Comment