Mambo aliyo nifanyia Diamond hayawezi kunipotezea hadhi yangu: Zari. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday, 20 September 2017

Mambo aliyo nifanyia Diamond hayawezi kunipotezea hadhi yangu: Zari.

Baada ya Msanii wa muziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ kukiri kuzaa mtoto na mwanamitindo Hamisa Mobeto, hatimaye mama watoto wake Zari Hassan ‘Zari’ azidi kumuweka njia panda msanii huyo juu ya uhusiano wao.

Mwanamama huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram ameeleza kupokea ushauri uliotolewa na baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii.

“Watu wakiamua kuchepuka au  kudanganya ni sawa na kujipotezea muda, ingawa wanahisi wanakuchezea wewe, hivyo usikate tamaa na usijilaumu kwa ajili ya makosa ya wengine, maisha lazima yaendelee,”

“Mambo yaliyotokea hayawezi kunipunguzia hadhi yangu, usijilaumu kwa yaliyotokea, zingatia malengo yako na kufanya maisha yaendelee,” amesema.

Amesema kuwa yale yote yaliyosemwa katika sakata hili yanabaki yalivyo na muda huu anaamua kuyaweka kando na kuelekeza nguvu zake kwenye maandalizi ya sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.

Sakata hili limeibuka siku moja baada ya Zari kujibu mapigo katika mtandao wa Snapchat akionya asihusishwe na kitendo alichokifanya Diamond cha kuzaa na Mobeto.

Awali katika maelezo yake mwanamuziki Diamond amesema ameshazungumza na mpenzi wake huyo kuhusiana na mtoto aliyezaa na Hamisa na kwamba ameelewa na hakuna tatizo tena.

No comments:

Post a Comment