Klabu ya Simba SC yafanya mazoezi ya mwisho CCM Kirumba kabla ya kuikabili Mbao FC kesho. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday, 20 September 2017

Klabu ya Simba SC yafanya mazoezi ya mwisho CCM Kirumba kabla ya kuikabili Mbao FC kesho.

Kikosi cha Simba kimefanya mazoezi yake ya mwisho leo kabla ya kuivaa Mbao FC katika mechi ya Ligi Kuu Bara jijini Mwanza, kesho.

Simba imefanya mazoezi yake kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa kama ambavyo sheria za Fifa zinaagiza timu “mgeni” kufanya mazoezi kwenye uwanja utakaotumika kwa mechi, siku moja kabla.

Kikosi chote cha Simba kimeonekana kuwa fiti na tayari kwa ajili ya mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu.

Mbao FC wao wamekuwa wakifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Butimba kujiandaa na mechi hiyo.
Simba tayari wamecheza mechi tatu, wakishinda mbili na sare moja na mechi hiyo dhidi ya Mbao FC itakuwa ya kwanza nje ya Dar es Salaam kwa msimu huu.

No comments:

Post a Comment