RAISI MPYA WA TFF, KARIA AANZA KWA MKWARA MZITO. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Saturday, 12 August 2017

RAISI MPYA WA TFF, KARIA AANZA KWA MKWARA MZITO.

Muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi wa nafasi ya uraisi katika Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), Wallace Karia alipewa nafasi ya kutoa neno kwa familia ya soka.
Karia ambaye aliibuka na ushindi wa kishindo katika uchaguzi huo, aliapishwa muda mfupi baada ya kutangazwa kwa matokeo ikiwa ni utaratibu mpya, kisha akapata nafasi ya kutoa hotuba kwa ajili ya wanasoka.
Akizungumza huku akionekana kujiamini, Karia alisema huu ni muda wa kupambana na kushikana kuwa wamoja ili kupeleka mbele mchezo wa soka.
Karia ameonyesha kuwa mkali na kutotaka utani katika uongozi wake ambapo amesisitiza umakini na watendaji wake kufuata mipango ambayo watakuwa wakiipanga kwa faida ya soka la nchi ya Tanzania.
Amesema kuanzia sasa hataki ubabaishaji kwenye soka, ameeleza kuwa anataka watu ambao wapo makini kwenye kazi, hao ndiyo ambao atafanya nao kazi.
Aidha, amemshukuru Waziri Harrison Mwakyembe ambaye alikuwemo kwenye mchakato wa uchaguzi mwanzo hadi mwisho mkoani Dodoma, kwa kusema kuwa TFF itafanya kazi pamoja na serikali kwa kuwa imeonyesha nia ya kuwasaidia na imekuwa na TFF bega kwa bega.

No comments:

Post a Comment