MICHANGO YA MSIBA WAKO IMENISIKITISHA SANA : RAMMY GALIS - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Thursday 10 May 2018

MICHANGO YA MSIBA WAKO IMENISIKITISHA SANA : RAMMY GALIS

Msanii wa filamu nchini Rammy Galis ambaye aliwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na 'Masogange' amefunguka na kusema taarifa kuhusu michango ya msiba wa Masogange zimemsikitisha na kuahidi kufanya jambo kupitia kazi yao ya pamoja ambayo anategemewa kutoka siku za karibuni.
Rammy Galis amesema hayo kufuatia kuwepo kwa tetesi kuwa michango ya rambirambi ya msiba wa Masogange imepigwa na baadhi ya wasanii ambao walikuwa wakiratibu zoezi hilo 
"Sintofahamu ya mchango wa msiba wako zimenisikitisha sana, namuomba Mungu anisaidie ili niweze kutoa kile kitakacho barikiwa katika kazi ya mkono wangu na wako 'Hukumu', Sania yupo kwa niaba yako mpenzi, pumzika salama Agness" aliandika Rammy Galis 
Rammy Galis na Masogange walibahatika kufanya kazi pamoja kipindi ambacho walikuwa katika mahusiano na kufanikisha filamu  inayokwenda kwa jina la 'Hukumu' ambayo bado haijatoka, ambapo kwa mujibu wa Rammy Galis mapato ambayo yatapatikana kupitia filamu hiyo amekusudia kufanya jambo kumuenzi Masogange. 

No comments:

Post a Comment