MSIMDHARAU MUME WANGU KISA NI DANSA : AUNTY EZEKIEL. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Saturday, 19 May 2018

MSIMDHARAU MUME WANGU KISA NI DANSA : AUNTY EZEKIEL.

Muigizaji wa Bongo movie Aunty Ezekiel amewatolea povu zito watu wote ambao wamekuwa wakimdharau mpenzi wake lakini pia Baba wa mtoto wake Mose Iyobo kisa ni mchezo shoo.

Aunty Ezekiel ameweka wazi kuwa hapendezwi na dharau hizo kwani ingawa wao wanaweza wakawa wanamuona yeye kama Dansa tu lakini yeye anamuona kama mkurugenzi fulani.

Aunty alisema amekuwa akifuatilia kwenye mitandao ya kijamii na kuona watu wakimchukulia poa Iyobo lakini anawaambia tu, yeye kwake anamuona kama mkurugenzi.

"Waache kumchukulia poa Moze wangu. Mimi namuona kama mkurugenzi fulani hivi, wao wakiona mtuanacheza muziki hawajui kama ni kazi, hawathamini na kuonesha dharau tu mitandaoni”.

Mose Iyobo ni Dansa maarufu kutoka WCB ambaye kwa muda mrefu ameonekana kwenye steji na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz akiwa anakata viuno.

Aunty Ezekiel na Mose Iyobo walikutana miaka minne iliyopita na mara moja watu walianza kumponda Aunty kwa kutoka na Mose Iyobo jambo ambalo hakujali. 

No comments:

Post a Comment