Nyota wa Liverpool Mohamed Salah ameshinda tuzo ya Mwanasoka bora wa Mwaka (FWA), inayoandaliwa na waandishi wa habari za soka nchini Uingereza (Football Writers Association).
Katika tuzo hiyo Mohamed Salah alikuwa akishindana kwa karibu na nyota wa Manchester City Kevin De Bruyne, lakini ameibuka mshindi akimzidi kwa kura 20 kiungo huyo raia wa Ubeligji.
Salah raia wa Misri, akiwa katika msimu wake wa kwanza ndani ya Liverpool amefanikiwa kufunga mabao 43 katika mshindano yote hadi sasa. Salah amekuwa msaada mkubwa kwa timu yake akiiwezesha kufika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mapema mwezi uliopita Salah alishinda tuzo ya mchezaji bora wa kulipwa wa ligi kuu ya soka nchini England (PFA na sasa ameongeza tuzo hii nyingine ikiwa ni matokeo ya kiwanmgo chake bora alichokionesha msimu huu.
Msimu uliopita tuzo hii ilichukuliwa na kiungo wa Chelsea na Ufaransa N'Golo Kante. Salah atakabidhiwa tuzo hiyo kwenye hafla ya chakula cha usiku itakayofanyika usiku wa Mei 10 jijini London.
No comments:
Post a Comment