Lissu aondoka Nairobi kwenda Ubelgiji - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Friday 5 January 2018

Lissu aondoka Nairobi kwenda Ubelgiji

Nairobi. Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu ametoka Hospitali ya Nairobi nchini Kenya leo Jumamosi asubuhi kwenda nchini Ubeljiji kwa matibabu zaidi yakuurejesha mwiliwake katikahali yake ya kawaida.
Lissu ambaye pia niRais wa Chama cha Mawakiliwa Tanzania(TLS) ataondoka saa 2.30 asubuhi yaleo Jumamosi naNdege yaShirika la Kenya akiambatana namke wake, Alicia.
Lissu ametoka hospitalini hapo ikiwa baada ya matibabu aliyoyapata tangu Septemba 7 mwaka jana baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30nawatu wasiojulikana kwenye makazi yakeDodoma.
Mwanasiasahuyo amesindikizwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta nawatoto wake pacha, Augustino naEdward, ndugu zake, viongozi nawanachama wa Chadema.
"Nawashukuru sana madaktari wa hapa Nairobi nawale wa Dodoma wakiongozwanaKatibu Mkuu (wa wizara ya afya Profesa Mpoki Ulisubisya waliookoa maisha yangu," amesema Lissu kabla ya kupandishwa gari la wagonjwa
"Nakwenda Ubelgijikwa matibabu, nikirudi mapambano yanaendelea, nawashukuruni nyote mlioniombea, nawashukuruWakenya na serikaliyao ambaokwa miezi minnenikiwa hapa walinipa ulinzi wakati wote."
Akizungumza kwa msisitizo mbele yawabunge na wanachama wa Chadema waliokuwapo amesema "Chapeni kazi,mimi nitarudi kuendelezamapambano haya."
Kuhusugharama, Katibu Mkuu wa Chadema, DkVicent Mashinji amesema gharama za safari namatibabu zimegharamikiwana Chadema naTLS.
Wakati baadhi yawaliokuwapo hospitalini kumsindikiza Lissu uwanja wa ndege ni kakayake Alute Mghwai, mdogo wake, Vinceti Mghwai nandugu wengine.
Pia, DkMashinji, Naibu Makatibu Wakuu,John Mnyika (Bara), SalumMwalimu (Zanzibar).
Wengine walikuwapo niwabuge wa Chadema, Susan Kiwanga (Mlimba) naGodbless Lema (Arusha Mjini), John Heche (Tarime Vijijini), Rose Kamili (Viti Maalum), Anna Gideria (Viti Maalum).
Kwa niabaya familia, Alute amesema "Tunamwomba Mungu ajalie hukoanakokwenda akapatematibabu, kwani alivyokujahapa sivyo anavyoondoka na tunawashukuru wananchiwa Tanzaniana Kenya kwa ushirikiano wao."

No comments:

Post a Comment