FAMILIA ya Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, kupitia kwa msemaji wake Alute Mughwai Lissu, imekanusha taarifa zilizokuwa zikisambaa mitandaoni zikidai mbunge huyo anatarajiwa kurejea nchini wakati wowote baada kupona majeraha ya risasi anayotibiwa huko Ubelgiji.
Alute ambaye pia ni Mwanasheria wa kujiegemea, amesema Lissuanatarajiwa kufanyiwa operesheni nyingine hivi karibuni huku akitoa rai kwa Watanzania kuendelea kumchangia ili aweze kufanikisha matibabu yake ya awamu ya tatu anayoendelea kuyapata nchini humo.
No comments:
Post a Comment