WATU 7 WAFARIKI KWA MAFURIKO JIJINI DAR ES SALAAM - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Sunday, 15 April 2018

WATU 7 WAFARIKI KWA MAFURIKO JIJINI DAR ES SALAAM

mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam zimeleta madhara jijini humo .
Kamanda wa polisi kanda maalum jiini Dar es salaam Lazaro Mambosasa amethibitisha vifo hivyo, na kueleza kwamba mwili mmoja umekutwa ukielea kuelekea maeneo ya Jangwani jijini Dar es salaam.
Sambamba na hilo Kamanda Mambosasa amesema maeneo mengi jijini Dar es salaam yamejaa maji, na kuwataka watu kuwa makini wanapotumia barabara hasa sehemu zenye makorongo, na kuwaangalia zaidi watoto ambao wanapita mara kwa mara wakienda shule au wakiwa wanarudi kutoka shule.
“Watu wasijaribu maji, ukijaribu maji ujue utaondoka nayo, kwa hiyo watoto wetu wanapokwenda shuleni tuwasindikize, sehemu nyingi zenye makorongo kwa mfano kule Kinyerezi, kule Goba kule Makongo, zile shortcut zote maji yamejaa, watu wajiepushe kutumia njia hizo, watapoteza watoto wakiwa wanaenda au kutoka shule”, amesema Kamanda Mambosasa.
Jeshi la Polisi limesema litaendelea kutoa taarifa za sehemu mbali mbali kuhusu hali ya mvua, ambayo inaendelea kuathiri sehemu kubwa ya nchi.

No comments:

Post a Comment