MVUA YAUA WAWILI NA KUJERUHI WENGINE MWANZA. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Monday 9 April 2018

MVUA YAUA WAWILI NA KUJERUHI WENGINE MWANZA.

Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha zimezidi kuleta madhara nchini, Mwanza yaua watoto wawili na kujeruhi wengine watatu baada ya kudondokewa na ukuta wa nyumba wakiwa wamelala.
Akizungumza kutoka kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, Ahmed Msangi amesema watoto hao wamefariki majira ya usiku wakati wakiwa wamelala katika nyumba waliyokuwa wanaishi katika mtaa wa Buguku kata ya Buhongwa wilayani Nyamagana Jijini Mwanza.

Kamanda Msangi amewataja watoto hao kuwa ni Mariam Saimon (4) pamoja na Musa Baraka (2) hukyu majeruhi wakiwa watatu katika tukio hilo.

No comments:

Post a Comment