SIWEZI KWENDA KUMUONA SUGU WALA KUMPELEKA MTOTO GEREZANI : FAIZA ALLY. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Thursday 22 March 2018

SIWEZI KWENDA KUMUONA SUGU WALA KUMPELEKA MTOTO GEREZANI : FAIZA ALLY.

MWIGIZAJI wa Bongo Movies ambaye ni mzazi mwenza na Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi almaarufu Sugu, Faiza Ally amefunguka kuhusu kumpelekea mtoto gerezani kumuona baba yake huyo alikofungwa kwa miezi mitano.

Akizungumza baada ya kuulizwa kama ana mpango wa kumpeleka mwanaye akamuone baba yake gerezani Mbeya na kumjulia hali, Faiza alisema kuwa, hawezi kufanya hivyo kwa kuwa Sugu siyo ndugu yake.

“Siwezi kwenda kumuona Sugu wala kumpelekea mtoto akamuone gerezani kwa sababu kwanza siyo ndugu yangu, siyo rafiki yangu na siyo mpenzi wangu. Mapenzi yalishaisha zamani, amebakia kuwa baba wa mtoto, basi, hayo mengine siwezi kuyafanya kwa kweli,” alisema Faiza.

Sugu yupo katika Gereza Kuu la Ruanda mkoani Mbeya akitumikia kifungo cha miezi mitano aliyohukumiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Pombe Magufuli.

No comments:

Post a Comment