MAMA IRENE UWOYA AMFUNGUKIA MAZITO DOGO JANJA HANA ADABU.. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Monday, 19 March 2018

MAMA IRENE UWOYA AMFUNGUKIA MAZITO DOGO JANJA HANA ADABU..

Wakati Dogo Janja na mke wa Irene Uwoya wakiendelea kufurahia maisha ndoa, Mama mzazi wa Irene Uwoya, Neema Mrisho amefunguka kwa kudai hampendi Dogo Janja kwa sababu msanii huyo hana adabu.

Wiki moja iliyopita akiwa Clouds Media mwigizaji huyo alidai ameshindwa kumpeleka Dogo Janja kwa wazazi wake, kutokana na kuwa mama yake kuwa mtu wa kusafiri mara kwa mara.

Akiongea na na Gazeti la Mwananchi Jumatatu hii, mama Uwoya amesema hata wangeamua kwenda kujitambulisha asingewapokea kwa kuwa Dogo Janja hana adabu ndiyo maana amefunga ndoa bila hata kufuata taratibu.

Mama yake, Uwoya amezungumzia utetezi wa mwanaye kuwa hauna mashiko kwani hata kama anasafiri haiwezi kuwa hivyo mwaka mzima na kwamba, ukweli ni mtoto wake anajua wazi kuwa ndoa hiyo hawaitambui na hawamkubali Dogo kwa kuwa ni mtoto ambaye hana adabu.

“Yaani ndugu mwandishi sijui nisemeje na mambo haya sipendi sana kuyaongea kwenye media (vyombo vya habari) kwa kuwa haipendezi kubishana na mtoto uliyemzaa kwenye vyombo vya habari, kwani mwisho wa siku yule ni mtoto wetu tu pamoja na kufanya mambo ambayo hayajatupendezi lakini mwelewe kwamba ndoa hiyo sisi kama wazazi hatuitambui na hatutaitambua,” amesema mama huyo.

Hata hivyo, mama Uwoya amesema ndoa hiyo ibaki kutambuliwa na hao Irene aliowaita kuwa ni ndugu zake, waliokwenda kushiriki harusi yake na waliomfungisha na kwamba, licha ya wazazi kuwa Dar es Salaam,  wanashangaa walijitokeza ndugu ambao hawawajui kusimamia jambo hilo.

“Siku ambayo ndoa inafungwa ndugu zake na wazazi wake tulikuwapo lakini tulishangaa kuona kwenye mitandao kuwa amefunga ndoa na hata ilipozidi kuvuma na kumuuliza majibu yake ilikuwa kwamba, alikuwa anacheza movie hivyo tuliamua kuachana nalo kwa kuwa huwezi kumlazimisha mtu akwambie ukweli kwa kile anachokiamini yeye,”amesema.

No comments:

Post a Comment