Msanii wa muziki Bongo, Dogo Janja amefunguka mipango yake ya kuoa mke wa pili,Dogo Janja ambaye alimuoa Irene Uwoya mwaka jana ameiambia The Playlist ya Times Fm kuwa kuoa mke wa pili hadi wa nne ni moja ya mipango yake na atafanya hivyo kila baada ya miaka 10.
“Inshallah kuongeza wa pili, wa tatu, wa nane hapo ukishakaa vizuri kiuchumi na mwenzako aweze ameridhia,” amesema.
“Hata wanne sio mbaya hapo tunaongelea Mwenyenzi Mugu akitujalia uhai labda baada ya miaka 10 naweza kuongeza wa pili, ikifika miaka 10 tena naongeza, yaani nikifika miaka 50 pale niwe nimekamilisha wanne,” ameongeza.
Dogo Janja na Irene Uwoya waliripotiwa kufunga ndoa November 25, 2017, hata hivyo ni vigumu kutaja tarehe kamili kutokana na namna walivyoliweka suala hilo hasa kwa upande wa vyombo vya habari na mitandao.
Job Opportunity At Uganda Airlines- Security Manager
-
*About US:*
Uganda Airlines is the National Carrier of the Republic of Uganda based at
Entebbe International Airport. It is headquartered in Entebbe, Waki...
No comments:
Post a Comment