Dismas Ten azungumza haya juu ya kamusoko.. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Tuesday, 13 February 2018

Dismas Ten azungumza haya juu ya kamusoko..



Afisa habari wa Yanga, Dismas Ten amesema kuwa daktari wa timu hiyo Dr. Bavu ametoa ruhusa ya Kamusoko kutumika hivyo ni jukumu la benchi la ufundi kuamua kumchezesha kama atakuwa amefanya vizuri kwenye mazoezi.

Aidha kwa upande mwingine Dismass amesema timu hiyo itaendelea kuwakosa nyota wake wanne ambao ni Abdallah Shaibu, Donald Ngoma, Yohana Mkomola na Amisi Tambwe kutokana na kuendelea kuuguza majeraha.

Mchezo wa raundi ya kwanza kati ya Majimaji na Yanga SC uliopigwa mjini Songea, ulimalizika kwa sare ya 1-1 na leo timu zinakutana katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu.

Yanga kwasasa ina alama 34 katika michezo 17 ikiwa katika nafasi ya pili huku Majimaji ikiwa na alama 14 katika nafasi 14.

No comments:

Post a Comment