Lwandamina,Pluijm wateta mazoezini - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Sunday, 14 January 2018

Lwandamina,Pluijm wateta mazoezini

Kocha wa zamani wa Yanga, Hans Pluijm ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha Singida United, alitumia muda wake kuwasalimia wachezaji wa Yanga na baadhi ya viongozi wa benchi la ufundi akiwamo Kocha George Lwandamina.

Makocha hao wawili walionekana wakibadilishana mawazo wakati timu zao zikipishana asubuhi kwenye Uwanja wa Uhuru mahali ambako zinafanyia mazoezi kujiandaa na michezo ya Ligi Kuu.

Kikosi cha Singida kinaendelea na maandalizi yake dhidi ya Simba ambayo ipo kileleni ikiwa imejikusanyia pointi 26 nao Singida United wakiwa kwenye nafasi ya tatu na alam 23.

Mazungumzo hayo ya kawaida kwa makocha hayo ilidhihirisha jinsi ambavyo viongozi hao wanauhusiano mzuri.

No comments:

Post a Comment