MWANAMUZIKI aliyejizolea jina kubwa kupitia wimbo wake wa ‘Majanga’ Snura Mushi amefunguka kuwa anatarajia kujipa tuzo ya kupambana mwenyewe kwenye maisha akiwa kama baba na mama kwa wakati mmoja.
Akizungumza Snura alisema kuwa, wanawake wengi siku hizi wamekuwa wapambanaji peke yao hivyo basi siyo vibaya kujitukuza.
“Kulea familia mwenyewe siyo kazi ndogo na siku hizi wanawake wengi tunapitia hili hivyo mimi mwenyewe najiandalia tuzo kabisa angalau nijipe moyo nizidi kutafuta kwa ajili ya wanangu,” alisema Snura
No comments:
Post a Comment