Chirwa amewaburuza Ajibu na Nyoni - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Thursday 9 November 2017

Chirwa amewaburuza Ajibu na Nyoni

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa amechaguliwa Mchezaji Bora wa Oktoba akiwa washinda beki wa Simba, Erasto Nyoni wa Simba na mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajib wa Yanga

Chirwa atazawadiwa Sh 1 milioni kwa kuibuka Mchezaji Bora baada ya kuwashinda wenzake wawili, beki wa Simba Nyoni na mshambuliaji Ibrahim Ajibu wa Yanga alioingia nao fainali katika uchambuzi uliofanywa na
Kila mwezi Kamati ya Tuzo za VPL ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) inapokea majina matatu ya wachezaji waliopendekezwa na makocha waliopo viwanja mbalimbali ambavyo ligi hiyo inachezwa msimu huu.

Mzambia huyo alitoa mchango mkubwa kwa Yanga mwezi uliopita ikipata pointi saba katika michezo mitatu iliyocheza na kupanda katika msimamo wa ligi kutoka nafasi ya sita iliyokuwepo Septemba hadi ya pili mwishoni mwa Oktoba.

Yanga iliifunga Kagera Sugar mabao 2-1 Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, ambapo Chirwa alifunga bao moja na kutoa pasi ya mwisho ya bao moja, pia Yanga iliifunga Stand United mabao 4-0 Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, ambapo Chirwa alifunga bao moja na kutoa pasi ya mwisho ya bao moja.

Kiwango cha mchezaji huyo kilionekana pia katika mchezo wa watani wa jadi Yanga na Simba uliofanyika Oktoba 28, 2017 Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya bao 1-1. Bao la Yanga lilifungwa na Chirwa, hivyo kwa mwezi huo alifanikiwa kuwa na kiwango cha juu katika kila mchezo ikiwa ni pamoja na kufunga.

Kwa upande wa Erasto naye alitoa mchango mkubwa kwa Simba uliowezesha timu hiyo kupata pointi nane katika michezo minne iliyocheza, akitoa pasi za mwisho za mabao nne, ambapo Simba ilishinda michezo miwili na kutoka sare miwili.

Ajib alitoa mchango kwa Yanga ikiwa ni pamoja na kufunga mabao matatu na kutoa pasi ya mwisho ya bao moja.

Wachezaji wengine ambao tayari wameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa mwezi wa VPL msimu huu ni mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi (Agosti), beki wa Singida United, Shafiq Batambuze (Septemba).

Kampuni ya Vodacom inayodhamini wa ligi hiyo ina utaratibu wa kuwazadiwa wachezaji bora wa kila mwezi, huku pia mwisho wa msimu kukiwa na tuzo mbalimbali zinazohusu ligi hiyo, ambapo msimu wa mwaka 2016/2017 kulikuwa tuzo 16 zilitolewa kwa washindi wa kada mbalimbali.

No comments:

Post a Comment