Tizi la Mrundi lawapagawisha wachezaji Simba - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Saturday 21 October 2017

Tizi la Mrundi lawapagawisha wachezaji Simba

WACHEZAJI wa Simba wameukubali mzuka wa Kocha mpya msaidizi, Masud Djuma. Kocha huyo kijana raia wa Burundi aliwasili nchini juzi alhamisi na jioni yake akatambulishwa na kuanza mazoezi na kikosi hicho.

Lakini aina yake ya utendaji imeonekana kuchangamsha mazoezi ya Simba ambapo wachezaji wanamuona kama mwenzao na wamekuwa wakifanya mazoezi kwa nguvu zaidi. Kocha Mkuu, Joseph Omog amekuwa akimpa maelekezo kisha kumuachia aendelee na mambo yake. Katika kila ambacho kocha huyo anataka wachezaji wakifanye amekuwa akikifanya kwanza yeye kama mfano iwe kupiga shuti, kukimbia, chenga, pushapu, chochote kile lazima na yeye afanye. Na ameonekana yuko fiti kimazoezi.

Katika mazoezi ya siku mbili Alhamisi ambayo yalifanyika katika uwanja wa Uhuru na Ijumaa Gymkhana wakiwa Mrundi huyo wachezaji wameonekana kuongeza nguvu zaidi ya kujituma.

“Kocha yupo vizuri kwani hata alipokuwa anatoa mazoezi ya kufanya alikuwa anatuelekeza na mwenyewe alikuwa anafanya ile inachangia kwa mchezaji kuongezeka kwa morali ya kufanya zaoezi analotoa mara mbili yake,” alisema Winga wa Simba, Jamali Mnyate
Lakini kinachoonekana ni kwamba kwenye mechi ya leo dhidi ya Njombe Mji kwenye Uwanja wa Uhuru, kocha huyo atamuanzisha Mavugo kwenye ushambuliaji.Mavugo ambaye tangu kuanza kwa msimu huu amekuwa na nafasi finyu katika kikosi cha Simba, ameshindwa kufunga bao hata moja. 

Vyombo ya habari mbalimbali vili shuhudia mazoezi ya Simba na kuona Mavugo akichezeshwa pamoja na kinara wa mabao wa Emmanuel Okwi katika kushambulia na kocha Masud alikuwa mkali pindi wanapokosea au kukosa nafasi ya wazi.

Huenda Mavugo alikuwa akichezesha na Okwi na pindi anapokosea alikuwa akikalipiwa anaweza kuingia katika kikosi cha kwanza moja kwa moja kwa kuwa katika mechi ya leo Simba watamkosa straika wao John Bocco aliyeumia kisigino kwenye mechi iliyopita dhidi ya Mtibwa.

Mazoezi ya jana, Masud alisimamia yote tangu walipoanza hadi kumaliza huku Omog akitoa maelekezo ya jumla kwa wote

No comments:

Post a Comment