Uongozi wa Simba umesema hautamuuza Kichuya kwa hasara kwa timu inayomtaka hadi hapo watakapoongeza kiasi cha pesa wanachotaka.
Simba imeahirisha mpango wake wa kumuuza kiungo wake Shiza Kichuya kwenye moja ya klabu kutoka falme za kiarabu kutokana na dau dogo.
Kiongozi wa juu, wa klabu hiyo amesema , awali walikuwa tayari kufanya biashara na klabu hiyo lakini baada ya kutaja dau dogo na wamegoma kuongeza tumeona nivyema tukaachana na mpango huo.
“Kichuya ni mchezaji mkubwa ndani ya Simba hivyo hatuwezi kumtoa kirahisi kama wanavyotaka wao kama wameshindwa kutoa kiasi cha pesa ambacho tumewaambia nivyema tukaahirisha,”amesema kiongozi huyo.
Kiongozi huyo amesema mchezaji huyo ataendelea kuichezea Simba na timu ambayo itakuwa tayari nivyema wakaonana na uongozi ili kupata thamani halisi ya mchezaji huyo.
Huu ni msimu wa pili kwa Kichuya kuichezea Simba, baada ya kuwa na msimu mzuri kwa na kuisaidia timu hiyo kurudi kwenye michuano ya kimataifa kwa kutwaa taji la Kombe la FA.
No comments:
Post a Comment