Taarifa za maendeleo ya Donald Ngoma baada ya kupata majeraha katika misuli ya miguu. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Tuesday, 3 October 2017

Taarifa za maendeleo ya Donald Ngoma baada ya kupata majeraha katika misuli ya miguu.

Mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma jana hakufanya mazoezi pamoja na wachezaji wengine kutokana na majeraha ya msuli aliyoyapata siku ya mechi ya Jumamosi wakati Yanga ilipocheza dhidi ya Mtibwa Sugar.

Ngoma alipewa saa 24 hadi 48 za uangalizi chini ya daktari wa Yanga ili kuona maendeleo kabla ya kutoa majibu kama anaweza kurudi uwanjani mapema au vinginevyo.

Leo asubuhi baadhi ya media zimezungumza na Godlisten Chicharito ambaye yupo kwenye timu ya kitengo cha habari ndani ya Yanga ambapo amesema, hali ya Ngoma inaendelea kuimarika.

“Jana hakufanya mazoezi alikuwa chini ya uangalizi wa daktari kuona maendeleo ya jeraha lake. Lakini kwa sasa anatembea vizuri ukilinganisha na ilivyokuwa mwanzo, anaweza kufanya mazoezi binafsi ikiwa ni tiba ya jeraha lake”-Chicharito.

Yanga inakabiliwa na mchezo wa VPL dhidi ya Kagera Sugar October 14, 2017 kwenye uwanja wa Kaitaba, mkoani Kagera.

No comments:

Post a Comment