Samatta,Msuva utawapenda tu! - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Monday 16 October 2017

Samatta,Msuva utawapenda tu!

Dar es Salaam. Washambuliaji wa Taifa Stars, Saimon Msuva wa Difaa El Jadidi (Morocco) , Abdul Hilal wa Tusker (Kenya) na Mbwana Samatta wa KRC Genk (Ubelgiji) wameing’arisha bendera ya Tanzania katika soka la kimataifa wiki hii.

Msuva ameiongoza Difaa kufuzu kwa nusu fainali ya Kombe la Mfalme ‘Throne Cup’ kwa jumla ya mabao 3-2, kwenye mchezo wa robo fainali ya kwanza uliuochezwa Oktoba 11 Difaâ ilipoteza ugenini kwa mabao 2-1 huku Msuva akifunga bao pekee.

Siku tatu baadaye (Jumamosi), Difaa ilicheza mchezo wa marudiano ya robo fainali ya pili kwenye uwanja wake wa nyumbani, Ben Ahmed El Abdi na kushinda mabao 2-0, Msuva alikuwa chachu ya upatikani wa matokeo hayo kwa kupika bao la kwanza dakika ya 64 lililofungwa na Adnane El Ouardy, la pili lilifungwa na Hamid Ahadad.

Msuva ameendelea kutumika akiwa mshambuliaji wa kati ambaye muda mwingine huwa huru kucheza hata pembeni.

“Nilianza mbele kabisa lakini kadri muda ulivyokuwa unasogea nilikuwa napewa maelekezo ya kuwa huru kwenye eneo hilo kwa maana ya muda mwingine kuja chini kuchukua mipira, kuvuta pembeni kama naona kuna nafasi ambayo inaweza kuwavuta mabeki wao wa kati ili kuachiwa mwanya.

“Nimeifurahia hiyo nafasi kwa sababu imenifanya niucheze sana mpira, tangu nitue huku nimekuwa nikiufurahia zaidi mpira kwa namna ninavyo chezeshwa, kilichopo mbele ni kuendelea kupigania matokeo na ikiwezekana itapendeza kama tutashinda hili taji,” alisema Msuva.

Nahodha wa Taifa Stars, Samatta ameiokoa KRC Genk  kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Royal Excel Mouscron katika mchezo wa Ligi Kuu Ubelgiji.

kwa kutengeneza nafasi ya bao la kusawazisha lililofungwa na
Genk iliyokuwa nyumbani, Luminus Arena ililazimika kusawazisha bao dakika 81, lililofungwa na Marcus Ingvartsen akimalizia pasi ya Samatta awali wageni Royal Excel Mouscron ilipata bao dakika ya 42, kupitia kwa winga Dorin Rotariu.

Kocha wa Genk, Albert Stuivenberg ameonekana akibadili mfumo wa timu hiyo uliozoeleka wa 4-2-3-1 na kuhamia kwenye 3-4-3, kwenye mfumo wa awali ni Samatta aliyekuwa akisimama kama mshambuliaji wa misho.

Mabadiliko hayo yameongeza idadi ya washambuliaji ambapo kwenye watatu wa mbele ni Samatta, Alejandro Pozuelo na Ingvartsen, watatu hao wamekuwa wakicheza kwa kubadilishana nafasi.

Abdul Hilal wa Tusker ameisaidia timu yake kupata pointi tatu muhimu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Kenya kwa kutengeneza mabao mawili kati ya manne waliyoshinda dhidi yaa Muhoroni Youth.

“Niliingia kipindi cha pili na kutengeneza mabao hayo, ushindi huo umetufanya tusogee mpaka nafasi ya tatu, tuna pointi 46, Sofapaka ambayo ipo nafasi ya pili imetuzidi pointi mbili na Gor Mahia inayoongoza Ligi na pointi 60 imetuzidi 14,” alisema Hilal.

Kinda Michael Lema bado yupo kikosi B cha Sturm Graz akitafuta ufiti kutokana na majeruhi aliyopata alishindwa kukukisaidia kikosi hicho kwenye mchezo waliocheza Jumamosi ambapo walipoteza kwa bao 1-0.

Lema ataingoza tena leo Sturm Graz II kwenye mchezo wa Ligi daraja la nne ambapo kikosi chao B kitacheza na Pasching/LASK Linz II,ugenini.

Kati ya wachezaji wa Kitanzania wanaocheza soka la kulipwa nchini Oman, Elius Maguri wa Dhofar na Salum Shebe Al-Mudhaibi hakuna anayeweza kumpa pole mwenzake baada ya wote kukutana na vipigo tofauti.

Al-Mudhaibi ya ilikuwa nyumbani, Al-Seeb Stadium ambapo imefungwa mabao 2-0 na Al Salam hivyo kuendelea kukalia kuti kavu kwenye msimamo wa Ligi hiyo ambayo ipo nafasi ya mwisho na pointi 3.

Dhofar ya Maguri yenyewe pengine inachakujitetea kwa sababu ilikuwa ugenini, Sohar Regional Sports  ambapo imefungwa bao 1-0 na Al Suwaiq, matokeo hayo yameifanya timu yake kushuka mpaka nafasi ya 6 na pointi 8
Licha ya timu ya kiungo  Mtanzania Said Mhando wa Chiasso ya daraja la kwanza, Uswizi kutangulia kwa bao 1-0 ilijikuta ikimaliza ya wenyeji wao, Neuchatel Xamax kwa mabao 4-1, Mhando aliingia kwenye mchezo huo dakika ya 68 kuchukua nafasi ya Orlando Urbano.

Naye Abdi Banda wa Baroka FC  ya Afrika Kusini ataendelea kuipigania timu yake kesho (Jumatano) kwenye mchezo wa Ligi ‘PSL’ watakapocheza na Golden Arrows, mchezo huo utakuwa saa 2;30 kwa mujibu wa saa za Afrika Mashariki.

No comments:

Post a Comment