Msanii wa filamu nchini Irene Uwoya amefunguka na kuweka wazi juu ya tetesi iliyopo mtaani kuhusu kuolewa na msanii wa muziki wa bongo fleva Dogo Janja na kusema ni kweli ameolewa na msanii huyo kwani ndiye mwanaume wa ndoto yake.
Irene Uwoya kupitia mtandao wake wa Instagram amethibitisha hilo na kusema kuwa anampenda sana msanii huyo na kudai huyo ndiye mwanaume wa ndoto yake hivyo anafurahi kuona wamefunga pingu ya maisha.
"Nimeolewa na mwanaume wa ndoto zangu, bado naendelea kulia na kutokwa na machozi ya kwa furaha.
Dogo Janja nakupenda sana na nimefurahi kumaliza maisha yangu ya duniani nikiwa na wewe" aliandika Irene Uwoya.
Kufuatia ujumbe huu ni wazi kuwa Irene Uwoya atakuwa amejibu maswali ya watu wengi ambao walikuwa hawaelewi nini kinaendelea kufuatia tetesi kuwa watu hao wamefunga ndoa siku za karibuni.
No comments:
Post a Comment