Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa amezua hofu katika timu yake baada ya kupata maumivu wakati wa mazoezi ya jana ya timu hiyo ikijiandaa na mchezo dhidi ya Stand United.
Mshambuliaji huyo alifanya mazoezi peke yake lakini baada ya muda mfupi alitoka nje akipatiwa matibabu ndani ya basi la timu hiyo akishindwa kurudi uwanjani.
Akizungumzia hali hiyo kocha mkuu wa Yanga, George Lwandamina amesema aliamua kumpumzisha Chirwa baada ya kupata majeraha katika mchezo uliopita na bado hajapona sawasawa.
Lwandamina alisema mazoezi ya timu hiyo sasa ni magumu na nguvu kubwa inatumika ambapo endapo Chirwa angeingia na kucheza angeweza kupata maumivu zaidi jambo ambalo hawataki kufanya makosa kwa kuliruhusu litokee.
"Tunamuhitaji Chirwa siku zote amekuwa ni mtu anayependa mapambano, lakini kama tukimchezesha wakati tunaona anahitaji muda kupona vizuri," alisema Lwandamina
No comments:
Post a Comment