MKASA MZIMA WA MWIZI ALIYE ROGWA NA KUBAKI NA MZIGO KICHWANI - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Thursday 3 May 2018

MKASA MZIMA WA MWIZI ALIYE ROGWA NA KUBAKI NA MZIGO KICHWANI

Mkazi wa Mbezi, Dar es salaam, Frank Japhet (23) amelazimika kujisalimisha kituo cha polisi Mlandizi, Kibaha, mkoa wa Pwani, baada ya mzigo wa mahindi unaokadiriwa kuwa na uzito wa kg 20, anaodaiwa kuuiba kung’ang’ania kichwani.
Kwa maelezo ya mtuhumuwa huyo aliyoyatoa kituoni hapo, mzigo huo wa mahindi kwenye gunia aliuiba kwa mama mmoja eneo la mtaa wa Nyambwiro, Mlandizi, Kibaha, Pwani majira ya saa 7.00 usiku wa kuamkia May 3 2018
Amesema alipoondoka na mzigo huo hadi eneo la stendi ya Mlandizi alipokuwa auache kwa mwenzake ili arudie mzigo mwingine, mzigo huo uling’ang’ania kichwani ambapo alijitahidi kuutoa kwa mbinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kulala ili akinyanyuka ubaki chini lakini ikashindikana.
Baada ya kuzunguka nao kwa muda mrefu alichoka hivyo akalazimika kujisalimisha polisi ili asije akauawa na raia wenye hasira watakapobaini kuwa ni mwizi .

No comments:

Post a Comment